Habari

Nyumba yaungua kimiujiza Dar

Chanzo cha moto mkali uliosababisha nyumba moja Jijini kuungua jana na kuteketeza kila kilichokuwamo ndani kimetajwa kuwa ni muujiza ambao hadi sasa haueleweki ulikotokea.

Na Sabato Kasika, Jijini



Chanzo cha moto mkali uliosababisha nyumba moja Jijini kuungua jana na kuteketeza kila kilichokuwamo ndani kimetajwa kuwa ni muujiza ambao hadi sasa haueleweki ulikotokea.


Mmiliki wa nyumba hiyo namba 67, iliyopo pale kwa Bibi Nyau, eneo la Magomeni Makanya, ameiambia Alasiri kuwa hadi sasa, anachoamini ni kwamba nyumba yake hiyo imeungua kwa sababu ya mambo ya kimazingara na si vinginevyo.


“Nimechanganyikiwa kwa kwakeli… sielewi ni kwa vipi imeungua maana sote tulikuwepo na hakuna kilichoonekana kuwa ni tatizo mchana huo,“ akasema Bi. Zalia Mohamed, mmiliki wa nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto jana, mishale ya saa 7:15.


Akasema mmiliki huyo kuwa moto uliounguza nyumba yake ulitokea ghafla na kwa kasi kubwa kiasi kwamba wao, licha ya kujitahidi kuuzima, kamwe hawakufanikiwa na badala yake wakapoteza kila kilichokuwamo.


“Nadhani ni moto wa mauzauza, si bure hata kidogo. Uliwaka ghafla kutokea kwenye chumba kimoja na ukateketeza nyumba kwa kasi ya ajabu,“ akasema kwa uchungu Bi. Zalia.


Akasema wakati moto huo ukitokea, yeye na baadhi ya wanafamilia wake walikuwa uani wakiendelea na shughuli za kupika.
Akasema, mara wakapatwa na harufu ya kitu kinachoungua ndani ya nyumba.


Akasema mmoja wao alienda ndani kujua kulikoni, nda ndipo akagundua kuwa kuna moto unawaka katika moja ya vyumba vya nyumba hiye yenye vyumba sita.


Baada ya hapo, akasema wakapiga kelele za kuomba msaada wa majirani huku nao wakifanya jitihada za kuudhibiti moto huo bila ya mafanikio.


Mwishowe, moto huo ulidhibitiwa na Kikosi cha Zimamoto kilichofanya kazi kubwa na gari lao namba STK 2691 waliokuwa pia wakisaidiwa na polisi waliokuwa na Difenda T 213 AMV, ambao waio, walizuia vitendo vya wizi.


Hata hivyo, tayari nyumba hiyo ilikuwa imeshaungua na karibu vyote vilivyokuwamo kuteketea.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents