Nyumba za wageni ziweke kamera kunasa matukio-Kova

surv_camera_m.jpgKamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova, amezitaka hoteli zote na nyumba za kulala wageni kuweka kamera za kunasa matukio

 


Na Anneth Kagenda

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova, amezitaka hoteli zote na nyumba za kulala wageni kuweka kamera za kunasa matukio.

Amesema kamera hizo zitakazokuwa zinaonyesha watu wanaoingia na kutoka hotelini hapo zitakabiliana na ujambazi ulioshamiri wa kutumia silaha.

Kadhalika, amewataka wahudumu wa nyumba hizo kuvaa sare na vitambulisho ili waweze kutambulika kwa urahisi kuwa yupi ni muhudumu na yupi ni ngeni.

Kamanda Kova alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni na madereva taksi, uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kuimarisha usalama katika maeneo yao.

Vile vile aliwataka wamiliki wa hoteli hizo kuweka vitabu kwa ajili ya kuandika majina ya watu wanaoingia.

Alisema wako watu ambao wanakawaida ya kutoandika majina yao kwa vile wanafahamiana na wamiliki hao na kwamba wanashutumiwa kuwa ni miongoni wa majambazi wanaofugwa ndani ya nyumba hizo.

“Agizo hili nalitoa kwa vile wako wanaofika katika hoteli zenu na kujifanya wateja kumbe wamefika kwa ajili ya kufanya uhalifu na kuiba mali za watu na ukiangalia jina lake kwenye kitabu hulioni hivyo nikisema kuwa wamiliki wanakuwa wanawajua nakuwa sijakosea,“ alisema Kamanda.

Aidha, alisema ikiwa wamiliki hao watafanya hivyo basi ujambazi wa kujificha kwenye nyumba hizo unaweza kupungua.

“Nyumba hizo huwa zinatuhumiwa mara kwa mara kwa kuwalea majambazi na mizigo ya wageni inaibiwa mara kwa mara hivyo iwapo tutashirikiana na jeshi la polisi nina imani uhalifu utapungua kwa kiasi kikubwa,“ alisema Kamanda Kova.

Kwa upande wa madereva taksi, Kamanda alisema kuanzia leo ndio mwisho wa magari yasiyosajiliwa kufanya biashara ya teksi jijini Dar es Salaam, na kwamba baada ya leo gari litakaloonekana likikaidi amri hiyo likamatwe mara moja.

Aliongeza kuwa ikiwa mtu anataka kufanya biashara hiyo basi asajili gari kwa utaratibu uliowekwa na si kutumia usafiri huo bila vibali kwa sababu magari hayo yanashutumiwa kwa kuwabeba majambazi na wauzaji wa madawa ya kulevya.

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents