Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nywele zamfikisha Marouane Fellaini jarida la GQ Style

Mchezaji wa klabu ya soka ya Manchester United, Marouane Fellaini, ataonekana katika jarida la GQ Style ambalo linatarajiwa kutoka wiki hii.

Fellaini anatokea kwenye jarida hilo kutokana na muonekano wake wa nywele ambazo amezoea kuzifuga kwa mtindo unaofahamika kama Afro. Mchezaji huyo Jumamosi iliyopita alifanikiwa kucheza mchezo wake wa 150 akiwa na Man United ambapo United waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW