Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

O-Ten naye awamwaga Wadosi..

Msanii O-Ten kutoka team ya East Coast Army iliyopo Upanga jijini Dsm, amepanga kutoingiza albam yake mtaani ili angalau mkwanja wake utokane na makusanyo ya milangoni katika maonyesho yake na hii ikiwa ni namna moja au nyingine ya kuwakwepa wezi wa kazi za wasanii ’Wadosi’.


Akiongea na chanzo chetu cha habari O-Ten ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kufiwa baba yake mzazi huko mkoani Morogoro,amesema atakuwa akirekodi ‘single’ na kuzipigia ‘promo’ kabla ya kwenda kuzitumia katika maonyesho yake ili kukwepa kufaidisha wasambazaji waliozoea kutumia jasho la wasanii kwa manufaa binafsi.

Akiendela anasema…”Sina mpango tena wa kuumiza kichwa na kupoteza gharama nyingi katika kuandaa albamu itakayomfaidisha ‘Mdosi’ wakati mimi niliyeumia nikibaki kuwa hohehahe,”.

Amesema kuwa uzoefu alioupata kwa takriban miaka minne ndani ya biashara ya muziki, ameweza kubaini kuwa mapato yanayotokana na shoo wanazofanya wasanii yanalipa kuliko kiasi kidogo cha pesa wanachopewa na wasambazaji kwenye mauzo ya albam.

”Sasa kama ‘singo’ moja ninayoiandaa kwa pesa ndogo inaniingizia zaidi kuliko albamu.. ina haja gani kujiumiza kuandaa albam yote?” akahoji.

Akionekana kuunga mkono kampeni iliyotangazwa hadharani na memba mwenzake A Y wa kundi la rap la East Coast Team, 0- Ten amewashauri na wasanii wengine nchini
kuweka rnsimamo kama huo hadi mafao yatakakapofanana na jasho wanalovuja.

Wasanii wengine waliotangaza kutofyatua albam ni Albert Mangwair, AY na GK huku mmiliki wa studio ya Dreams Multirnillion Record, Najmuddin Said, akitangaza kusambaza mwenyewe albam ya wasanii wake wanaochipukia kwa
kuiwekea coupon zitakazokuwa na shindano la kuwania gari.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW