Habari

Obama alitoa onyo hili kwa Trump

By  | 

Imebainika kuwa Rais Barack Obama alimuonya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya kumteua Michael Flynn kuwa mshauri wake wa maswala ya usalama wa kitaifa.

Maafisa wa zamani wa Obama wamesema, Barack alionya juu ya uteuzi wa Flynn siku mbili baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana.

Katibu wa masuala ya habari, Sean Spicer alisema kwamba ni kweli Obama aliweka wazi kwamba hakupenda uteuzi wa Jenerali Flynn.

Lakini Spicer alisema kuwa hilo sio jambo la kushangaza kwa kuwa jenerali Flynn alikuwa amefanya kazi na rais Obama na kwamba alikuwa mkosoaji mkubwa wa rais huyo hususan kwa kushindwa kwake kuwa na mipango ya kulikabili kundi la IS na vikwazo vingine vilivyokuwa vikikabili Marekani.

Jenerali Flynn alijiuzulu nafasi yake mwezi Februari mwaka huu kwa kosa la kutoa baadhi ya taarifa kwa maafisa wa Urusi ikiwa ni wiki tatu tangu akalie kiti chake.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments