Siasa

Obama amgalagaza Romney kwenye mdahalo wa pili

Rais Barack Obama amerejea kwa kishindo dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney kwa kumfunika kwenye mdahalo uliofanyika alfajiri ya leo (Jumanne usiku kwa Marekani).

Mdahalo huo wa pili kati ya midahalo mitatu iliyopangwa kufanyika umewapa nguvu wanachama wa Democrats waliokuwa wana hofu baada ya Obama kufanya vibaya kwenye mdahalo wa kwanza wiki mbili zilizopita.

Obama ametetea sera zake na kumchallenge Romney kwa kubadilisha badilisha misimamo kwenye masuala muhimu na kudai kuwa sera za mpinzani wake zitawapendelea matajiri kama akichaguliwa.

Kwa mujibu wa kura za CNN, Obama amefanya vizuri kwa asilimia 46 dhidi ya Romney aliyepata asilimia 39.

Zaidi ya tweets milioni 7 zimeandikwa wakati wa mdahalo huo.

Hizi ni miongoni mwa tweets maarufu:

Michelle Obama ‏@MichelleObama

Obama akimkumbatia mke wake Michelle baada ya mdahalo
I’m so proud of my husband tonight. Let’s have his back as he has had ours. –mo #TeamBarack

Mr GONGA ‏@GongaCEO
Jamani mbona Bongo hatunaga Debabes Kama Hizi….. Inamaana Candidates wetu hawajiamini kujielezea mbele ya Umma? … http://m.tmi.me/yay5s

Deepak Chopra ‏@DeepakChopra
@BarackObama kept @MittRomney on the defensive & then knocked him down so hard he never recovered.

Maria Sarungi Tsehai ‏@MariaSTsehai
Mi niliwaambia kuwa in 1st debate Obama aliturusha roho makusudi – this mjaluo knows exactly how to debate.. subirini ya 3 mtashangaaa!
Leo Obama anaua kabisa lakini in a very firm polite manner… ROmney campaign said ‘We’ll get bck to you” on women equality

Zitto Zuberi Kabwe ‏@zittokabwe
Hongera Obama kwa kushinda mdahalo huu. Umefanya vizuri sana. Wanasiasa wasio wakweli lazima waumbuliwe kinaga ubaga.

Jeff Msangi ‏@BongoCelebrity
Kwenye issue ya Libya,Obama anajaribu kumwambia Romney,oyaa keep moving,utapata aibu,jamaa akajidai mjanja ikala kwake vibaya sana! #debate

Babu Sikare ‏@AlbinoFulani
Excellent answer on Benghazi. Sincerity and accountability. #Obama #Debate2012
Romney is gonna pay a huge price in a lil bit on facts check. #Debate2012

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents