Picha

Obama: Trump hafai kuiongoza Marekani

Rais wa Marekani anayeondoka madarakani, Barack Obama amewataka viongozi wa chama cha Republican kujiondoa kumuunga mkono mgombea urais wa chama hicho, Donald J. Trump kwa kumwelezea kama mtu asiyefaa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Barack Obama

Akiongea kwenye Ikulu ya White House, Obama alimkosoa vikali Trump kwa kuwashambulia wazazi wa kiislamu wa mwanajeshi wa Marekani, Capt. Humayun Khan, aliyeuawa nchini Iraq.

“Swali ambalo wanatakiwa wajiulize wenyewe ni: Kama wamekuwa wakirudia kusema kwa maneno makali kuwa anachosema hakikubaliki, kwanini bado mnamuunga mkono,” alisema Obama.
Tayari Trump ameshamjibu Obama kwa kumuit kuwa ni ‘janga.’

“Amekuwa dhaifu, amekuwa asiyejiweza,” alisema Trump kwenye mahojiano na Fox News Jumanne hii.

Baadhi ya viongozi wakubwa wa chama cha Republican wamejiondoa kumuunga mkono Trump. Mdhamini muhimu wa chama hicho, Meg Whitman amemuunga mkono wazi mgombea wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na kumkosoa Trump.

Kwa mujibu wa kura za maoni za Reuters/Ipsos, Hillary Clinton ameendelea kuongoza dhidi ya Trump kwa asilimia nane.

Naye Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Jumanne hii alimkosoa mgombea huyo kwa kudai kuwa amekuwa akiwafanya watu wajisikie kichefuchefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents