Habari

Oceania Cruises watangaza safari ya meli ya kuzunguka dunia kwa siku 180 katika nchini 44 kula bata, nauli ni TSH mil 64!

Una shilingi milioni 64 za kuchezea? Una siku 180 za kutembea duniani na kula bata? Kama unazo basi safari hii ya meli kubwa ya Oceania inakuhusu. Ni safari ya kwanza kwa urefu ya siku 180 kwenye meli hiyo Insignia.

insignia-owners-suite-1-600x450
Chumba

Meli hiyo itachukua wasafiri (wageni) 684 na itazunguka kwenye mabara 5, nchi 44 na kufika kwenye bandari 89.

lounge-1-600x450
Mgahawa

Safari ya Insignia itaanzia Miami, Marekani, kwenda visiwa vya Caribbean, Amerika ya Kusini, na kisha kwenda kwenye bandari 12 za Afrika.

ocean-view-1-600x450
Chumba

Safari hiyo itaendelea hadi barani Asia na kupitia kwenye nchi za India, Indonesia, Australia, New Zealand na kisha South Pacific na Hawaii.

veranda-stateroom-1-600x450

Meli hiyo ni ya kifahari na ina kila kitu ndani, vyumba vya kisasa, gym, casino boutique, bwawa kubwa la kuogelea, na Club.

vista-suite-1-600x450

Safari hiyo ya kuzunguka duniani itagharimu dola $39,999 sawa na shilingi milioni 64 kwa kila kichwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents