Burudani

Octopizzo: Kabla ya kufanikiwa, nilikuwa nikiagiza chakula hoteli, kula na kusepa bila kulipa

Mkali wa rap anayewakilisha mtaa wa Kibera-Kenya Octopizzo, Alhamis hii amefunguka kuhusu vitu ambavyo wengi hawakujua kumhusu.


Kupitia kipindi cha Mambo Mseto kinachoongozwa na Mzazi Willy Tuva wa Citizen Radio, Rapper huyo alifunguka baada ya kuulizwa kuhusu kitu ambacho aliwahi kukifanya ila mashabiki zake hawafahamu.

Octopizzo alisema kwamba wakati bado anahustle kabla ya kutoka kimuziki, alikuwa na tabia ya kuagiza msosi kwa mahoteli ya mtaa na baada ya kula anachomoka ghafla bila ya kulipa bili. Hii hapa ilikuwa ni taratibu yake kwa kuwa kipindi hicho maisha yalikuwa magumu kiasi cha kwamba asingeweza kukidhi baadhi ya mahitaji yake ya kawaida.

Kilichokuwa kikimkinga dhidi ya kuadhibiwa ni kwamba alikuwa yupo honest na pia kumshtaki mtu kwa kosa kama hilo haikuwa rahisi kwa kutokuwa na mantiki sawa. Octo aliendelea kwa kusema wakati mwingine alilazimika kutumia ujanja zaidi katika masuala hayo. Alisema kwamba alikuwa akiwabeba wadudu kama Mende hivi kwenye mfuko kisha anadunda pale hotelini na kuagiza chakula bora zaidi na kupiga msosi fresh.

Baada ya kutosheka basi anachomoa wale wadudu na kutia kwenye chakula kile na kuanza kulalamika ghafla. Inabidi pale waiter kufika na ndio hapo namuonesha chakula kikiwa na vidudu. “Inabidi aniombe msamaha na kushindwa kuitisha malipo kwa kuwa ni kitu ambacho kingefanya wapoteze wateja wengi tu,” alisema. Mara nyingi alikuwa akipewa chakula kingine bure.

Kwa sasa rapa huyo ana kazi mpya kwa jina ‘Tergat Gang’ ambapo ndani amewashirikisha Barack Jaccuzzi na Boutross ambao ni new rappers wanaoibuka vizuri.

By:Teddyza Agwa
Instagram @teddyzabway
+254710487436

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents