Habari

Octopizzo wa Kenya kupanda jukwaa moja na rapper wa Marekani 2 Chainz huko Uingereza

Hit maker wa ‘Ivo Ivo’ Octopizzo anazidi kudhihirisha ukomavu wake katika cheo chake kipya cha ‘ustaa’ baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha Kenya katika ‘UN-Convention Conference’, mkutano unaotegemewa kufanyika (September) mwaka huu huko Birmingham,Uingereza.

Octopizzo_ Octopizzo

Octopizzo ambaye alitoa habari hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook, anategemewa kupanda jukwaa moja na rapper wa Marekani 2 Chainz ambaye pia yuko katika orodha ya wasanii 33 wa kimataifa watakao perform.

chainz
2 Chainz

Rapper huyo wa Kibera Namba Nane Octopizzo ndiye msanii pekee wa Kenya aliyechaguliwa kuwakilisha nchi hiyo kati ya wasanii 33 wa kimataifa waliochaguliwa kuperform katika mkutano huo wenye lengo la kujenga uelewa juu ya mapambano ya vita na migogoro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents