Michezo

Odama na Rayvanny kuweka historia mpya jijini Tanga (+video)

Muigizaji wa filamu Odama na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny usiku wa leo wameahidi kutikisa jiji la Tanga kwenye uzinduzi wa ziara yao ya Mr. Kiongozi ambayo rasmi inzinduliwa leo.
https://youtu.be/5ITG7NMejxY

Akiongea na redio TK FM ya jijini Tanga, Odama ambaye ndiye muaandaji wa Tamasha hilo akishirikiana na Albabu Entertainment amesema kuwa uzinduzi huo utakuwa ni wa kihistoria na wa kipekee kwani watu wote watakaokata tiketi watapewa nakala moja ya filamu ya Mr. Kiongozi na kupiga picha na mastaa wote watakaopita kwenye red carpet.

Kiingilio cha show hiyo ni Tsh buku 10 na itafanyika katika ukumbi wa Nyumbani Hoteli jijini Tanga.hii ni show ya kwanza kufanyika jijini Tanga ya Wasanii wa filamu na muziki kupanda jukwaa moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents