Habari

Odinga ataka wafuasi wake kutoshiriki tendo la ndoa mkesha wa uchaguzi

Mgombea wa urais katika muungano wa NASA nchini Kenya, Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoshiriki tendo la ndoa mkesha wa siku ya uchaguzi.

Bwana Odinga amefananisha uchaguzi huo na vita akisema kuwa kushiriki ngono kabla ya kwenda vitani ni mkosi mbaya ambao unaweza kusababisha mtu kushindwa.

“Tunaenda vitani na lazima tuhifadhi nguvu yetu kabla ya siku ya vita ambayo ni Agosti 8”, alisema mjini Homabay eneo la magahribi mwa Kenya.

“Hakuna hata mmoja wetu ambaye anafaa kushiriki ngono kabla ya mkesha wa siku ya uchaguzi’.

Odinga hususan aliwasisitizia wanaume akisema itasababisha wengine wao kutopiga kura.

Wanawake alisema ,hawafai kukubali kushiriki katika tendo la ndoa na waume zao usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, alisema.

“Kila mwanamke anafaa kumnyima mumewe haki yake ya tendo la ndoa”,alisema.

Raila awaomba wafuasi wake kutoshiriki ngono mkesha wa uchaguzi

“Hatua hiyo itatufanya kuamka mapema alfajiri ili kupiga kura na kulinda kura na kuilinda siku nzima hadi pale kura zitahesabiwa na kutangazwa”.

Sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa chama cha ODM kukataza tendo la ngono wakati wa uchaguzi.

Wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za muungano wa NASA mjini Kakamega magharibi mwa Kenya , tarehe 3 mwezi Juni, Odinga aliwaambia wafuasi wake kusubiri hadi pale matokeo yatakapotangazwa ili kuweza kufurahia tendo hilo la ndoa.

“Nawaomba wanawake, kuwaambia waume zao kusubiri hadi baada ya uchaguzi ili kuweza kushiriki tendo hilo ili kusherehekea ushindi wetu”.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents