Burudani ya Michezo Live

Ofisi nyingine ya Serikali yachomwa moto na watu wasiojulikana, RC Morogoro atoa tamko kali ‘Salama yao watoke nje ya mkoa’

Yakiwa ni masaa machache yamepita baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Ofisi nyingine tena ya Kijiji Cha Mlali  wilayani Mvomero mkoani Morogoro nayo imechomwa moto na kuteketeza nyaraka mbalimbali za kiserikali.

Baadhi ya nyaraka zilizoteketea kwa moto.

 

Akiongea kwenye eneo la tukio hilo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare pamoja na kamanda wa polisi mkoa hu, Wilbroad Mutafungwa wamesema tayari wamewakamata watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye tukio hilo akiwemo Diwani wa kata hiyo, Frank Mwananjinje (CCM).

Akiongea kwenye eneo la Tukio, RC Ole Sanare amesema watu hao waliochoma ofisi hiyo watatafutwa popote pale walipo na salama yao wakimbilie mkoa mwingine.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW