Ofisi ya Bobi Wine yavamiwa, CCTV zachukuliwa (+Video)

Ofisi ya chama cha mgombea wa Urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine imevamiwa na makumi ya wanajeshi wenye silaha pamoja na maafisa wa polisi.

View this post on Instagram

OFISI YA BOB WINE YAVAMIWA, CCTV ZACHUKULIWA . Ofisi ya chama cha mgombea wa Urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine imevamiwa na makumi ya wanajeshi wenye silaha pamoja na maafisa wa polisi. Nyaraka zimeripotiwa kuchukuliwa kutoka kwenye ofisi pamoja na kofia yenye muundo wa kijeshi na magwanda vimechukuliwa. Kamera za CCTV pia zimechukuliwa. Mmoja wa washauri wa Bobi meiambia BBC kuwa maafisa hawakuwasilisha kibali walipokua wakiingia kukusanya nyaraka na mavazi. Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga ameiambia BBC, ‘tunafanya operesheni juu ya utumiaji mbaya wa sare za kijeshi. Septemba mwaka jana, serikali iliidhinisha kofia nyekundu sawa na anayovaa Bobi Wine na wafuasi wake ni sare ya jeshi-ikimaanisha kuwa yeyote anayeonekana ameimiliki au kuivaa kinyume cha sheria anaweza kushitakiwa. Bwana Enanga amesema operesheni inaendelea na kwamba maafisa watasaka maeneo mengine pamoja na ofisi za National Unity. Bobi Wine amesema kuwa nguvu za dola zinamlenga na chama chake wakati akijiandaa kukabiliana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021. Lakini msemaji wa polisi anasisitiza kuwa operesheni hiyo haijachochewa kisiasa. #Bongo5Updates

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Nyaraka zimeripotiwa kuchukuliwa kutoka kwenye ofisi pamoja na kofia yenye muundo wa kijeshi na magwanda vimechukuliwa. Kamera za CCTV pia zimechukuliwa.

Mmoja wa washauri wa Bobi meiambia BBC kuwa maafisa hawakuwasilisha kibali walipokua wakiingia kukusanya nyaraka na mavazi.

Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga ameiambia BBC, ‘tunafanya operesheni juu ya utumiaji mbaya wa sare za kijeshi.

Septemba mwaka jana, serikali iliidhinisha kofia nyekundu sawa na anayovaa Bobi Wine na wafuasi wake ni sare ya jeshi-ikimaanisha kuwa yeyote anayeonekana ameimiliki au kuivaa kinyume cha sheria anaweza kushitakiwa.

Bwana Enanga amesema operesheni inaendelea na kwamba maafisa watasaka maeneo mengine pamoja na ofisi za National Unity.

Bobi Wine amesema kuwa nguvu za dola zinamlenga na chama chake wakati akijiandaa kukabiliana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021.

Lakini msemaji wa polisi anasisitiza kuwa operesheni hiyo haijachochewa kisiasa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW