Uncategorized

Ofisi ya Rais wa Liberia yaingiliwa na nyoka, wafanyakazi waandikiwa barua ya kubaki majumbani kwao

Nyoka wamepatikana katika ofisi ya Rais wa Liberia George Weah , hatua iliomshinikiza kutoka na kwenda kufanya kazi katika afisi ya kibinafsi.

Tatibu wa maswala ya habari Smith Toby aliambia BBC kwamba siku ya Jumatano nyoka wawili weusi walipatikana katika jumba la ofisi ya wizara ya maswala ya kigeni .

Wafanya kazi wote wametakiwa kutoingia katika ofisi hiyo.

”Ni kuhakikisha kuwa wadudu wote wanaotambaa na kutembea wanaangamizwa katika jumba hilo”, alisema bwana Toby.

”Wizara ya maswala ya kigeni ndio ilio na ofisi ya rais, hivyo basi ikalazimika kuandika barua ikiwasihi wafanyakazi kusalia majumbani huku wakiendelea kuweka dawa hiyo”, alisema.

Kanda ya video iliochapishwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la African News ilionyesha wafanyakazi wakijaribu kushambulia nyoka wakati walipoonekana katika eneo la kukaribisha wageni la jengo hilo.

”Nyoka hao hawakuuliwa” , bwana Toby alisema. ”Kulikuwa na shimo mahali fulani ambalo walitumia kurudi”.

Maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa rais walionekana wakiyalinda makao ya bwana Weah katika mji mkuu wa Monrovia .

Msafara wa magari wa rais huyo ulionekana kuegeshwa nje ya jumba hilo.

Bwana Toby alisema kuwa wizara ya maswala ya kigeni ilianza kunyunyiza dawa hiyo siku ya Ijumaa.

inland taipan (picture-alliance/blickwinkel/R. Koenig)

”Jumba hilo limekuwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa sasa kwasababu yamfumo wa maji taka , hivyobasi kuna uwezekano wa nyoka kuingia katika jumba hilo”, alisema.

”Rais anarudi katika ofisi yake rasmi siku ya Jumatatu baada ya dawa hiyo kunyunyizwa, iwapo nyoka hao watapatikana na kuuawa au la”, alisema bwana Toby.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents