Michezo

Okwi aipoteza Singida United uwanja wa Taifa

By  | 

Kikosi cha klabu ya Simba kimefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya timu ya Singida United mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Katika mchezo huo Simba SC imeonekana kuutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa huku wachezaji Shiza Ramadhani Kichuya, Asante Kwasi na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi akitupia mawili na kuhitimisha karamu ya mabao.

Kwa mabao hayo mawili ya mshambuliaji Okwi anafikisha jumla ya magoli tisa na kuongoza katika msimamo wa magoli wakati nafasi ya pili ikishikwa na mchezaji wa Mbao FC, Haji Hamidu nafasi ya tatu ikienda kwa Obrey Chirwa wa Yanga SC na Shiza Kichuya wa Simba SC akiwa na idadi sawa na Chirwa.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuwa na alama 29 wakati nafasi ya pili ikishikwa na Azam FC wenye pointi 27 wakati nafasi ya tatu ikiwa ni Mtibwa Sugar.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments