Michezo

Ole Gunnar afunguka mbinu za kumdhibiti Messi na Suarez ‘tumewaweza Ronaldo na Mbappe, hatushindwi’ (+video)

Kocha wa klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameeleza kuwa leo kwenye mchezo wa Klabu bingwa dhidi ya Barcelona wamejipanga vya kutosha, hususani katika kuwadhibiti wasambuliaji hatari wa klabu hiyo, Lionel Messi na Suarez.

Image result for MESSI VS OLE GUNNAR
Messi na Ole Gunnar

Ole Gunnar akiongea na waandishi wa habari jana jioni April 9. 2019, Amesema kuwa safu yake ya ulinzi ipo tayari kukabiliana na washambuliaji hao, kwani ndani ya msimu huu imepambana na wachezaji wenye karba kama yao akiwemo Ronaldo na Mbappe pale wakati Man U ilipovaana na Juventus na PSG.

Kuhusu plan maalumu ya kumzuia Messi na Suarez, ni kweli hiyo ipo na Smalling ataangalia kila liwezekanalo. Hata hivyo ni jambo la kawaida tulifanya hivyo na tuliweza kwa Ronaldo na Mbappe, kwa akina Hazard.“ameeleza Ole Gunnar na kufafanua swali hilo aliloulizwa kuhusu mpango maalumu wa kumbana Messi.

Kiuhalisia hao (Messi na Suarez) ni moja ya wachezaji bora duniani kwa sasa, hivyo ni nafasi tu ndio tutakayoiangalia ya kuweza kuwadhibiti, huwezi kusema kumsimamisha Messi asiingie kwenye box kwani unaona mwenyewe anafunga magoli mangapi akiwa nje ya Box?,“amesema Ole Gunnar .

Kwa upande mwingine, Ole Gunnar amesema kuwa kumzuia Messi asipate goli inawezekana inagwaje sio kazi rahisi.

Leo Aprili 10, 2019 usiku Man United wanavaana na Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents