Michezo

Ole Gunnar aifikia rekodi ya Sir Matt ya zaidi ya miaka 70 Manchester United, baada ya ushindi wa jana



Kocha wa Manchester United Mnorway ameweka rekodi ambayo haikuwekwa kwa muda mrefu katika klabu ya Manchester United ambayo haikuwekwa kwa zaidi ya miaka 70.

Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Newcastle ambao unaifanya Manchester United kushinda michezo minne mfululizo baada ya kupata kocha mpya.


Mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku aliingia kama mchezaji wa ziada yaani superSub na kufunga na kufunga goli baada ya kugusa mpira kwa mara yake ya kwanza baada ya kuingia uwanjani na kuiwezesha Manchester United kuwalaza Newcastle United 2-0.

Rashford aliongeza bao la pili dakika ya 80 baada ya uchezaji wa kuridhisha ulioshirikisha Lukaku na Alexis Sanchez ambaye pia alikuwa ameanza mechi akiwa benchi.

Baada ya ushindi huo sasa raia huyo wa Norway ameifikia rekodi ya meneja maarufu Sir Matt Busby aliyefanya hivyo mwaka 1946, kwa kushinda michezo minne mfululizo akiwa kama kocha mpya aliyokabidhiwa timu.

Baada ya ushindi wa kuridhisha dhidi ya Cardiff, Huddersfield na Bournemouth, mechi hiyo ya Jumatano ilikuwa mtihani mkubwa zaidi kwa Manchester United chini ya Solskjaer.

Matokeo ya mechi za EPL Jumatano 2 Januari, 2019

  • Bournemouth 3-3 Watford
  • Chelsea 0-0 Southampton
  • Huddersfield 1-2 Burnley
  • West Ham 2-2 Brighton
  • Wolves0-2 Crystal Palace
  • Newcastle 0-2 Man Utd

By Ally Juma.



Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents