Uncategorized

Ole Gunnar awaomba radhi mashabiki wa United, ni baada ya kipigo kutoka kwa Everton

Meneja wa klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu yake kukubali kichapo kizito cha goli 4-0 toka kwa Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.

United wamepoteza jumla ya michezo sita ya hivi karibuni ikiwa ni mechi nane katika michuano yote waliyokuwa wakishiriki ikiwemo ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mchezo dhidi ya Everton ulikuwa ni muhimu sana kwa klabu hiyo katika mbio za kuwania nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.

” Nataka niombe radhi kwa mashabiki wote wa klabu hii tulizidiwa katika kila idara ila tulipata hamasa ya kutosha toka kwa mashabiki wetu na tutajitahidi kufanya vyema siku ya jumatano.” Hii ilikuwa Kauli ya Ole Gunnar Solskjaer, baada ya kumalizika kwa mchezo

Kwa Upande wake golikipa wa Man United David De Gea aliyekuwa nahodha katika mchezo huo amesema was ” Ni ngumu kuweka katika manene vile anavyojisikia baada ya kipigo hicho kikubwa toka Ole apewe jukumu la kuinoa klabu hiyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents