Soka saa 24!

Ole Gunnar Solskjaer akiri Manchester United bado inakazi ya kufanya baada ya kipigo cha PSG

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa timu yake bado inakazi ya kufanya akitumia neno ‘inamlima wa kuupanda’ kufuatia kipigo cha mabao 2 – 0 dhidi ya Paris St-Germain mchezo wa hatua ya 16 Champions League.

Solskjaer ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na BT Sport mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao ambapo alishuhudiwa aliyekuwa winga wa United, Angel di Maria akitoa pasi zilizochangia kupatikana kwa mabao yaliyofungwa na Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe.

”Huwezi kusema imekwisha, hapana ila bado na sisitiza ule mlima lazima lazima unapaswa kupandwa.” Amesema Ole Gunnar Solskjaer.

Kwa mchezo huo wapenzi wa United wameshuhudia kiungo wao, Paul Pogba akitolewa nje dakika zamwisho.

“Leo tumekutana na aina ya timu zenye levo za juu, hizi ndiyo levo ambazo tunataka kwenda. Kuwepo kwenye nne bora ni jambo moja lakini United inapaswa kuwepo kwenye timu bora. Wachezaji wetu sasa tunataka kusogea mbele.”

“Tuna wachezaji bora lakini hutupatia kitu fulani, wacha tuendelee kuwa na wacha tuwatumainie huwenda hawakuwa makini, wamekuwa na majeraha tuwape siku kadhaa.”

Huu ni mchezo wake wa kwanza kwa Solskjaer wa Kimataifa, ameshapata kucheza jumla ya michezo 11 ya ligi kuu Uingereza mpaka sasa na kufanikiwa kushinda 10 na sare moja akirithi mikoba ya Jose Mourinho aliyetimuliwa katikati ya mwezi Desemba.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW