Michezo

Ole Gunnar Solskjaer amtamani, Harry Kane, Unai Emery afunguka juu ya kiungo hatari wa Liverpool, Fabinho

Unai Emery amedokeza kuwa alikaribia kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na raia wa Brazil Fabinho, 26, alipojiunga na Arsenal kama kocha mkuu mwaka jana. (Evening Standard)

Fabinho

Manchester City imeongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 23, na pia ilituma wataalamu wake kufuatilia mechi ya Jumatano ya Champions League dhidi ya Red Bull Salzburg. (Guardian)

Tottenham inamfuatilia mshambuliaji wa Gremio raia wa Brazil Everton Soares, huku mtaalamu mkuu soka Steve Hitchen akimtazama mchezaji huyo wa miaka 23 katika michuano ya Copa Libertadores. (Sky Sports)

Manchester United ina mpango wa kuwasajili wachezaji wawili wa safu ya mashambulizi baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kuomba kuimarisha kikosi chake zaidi. (Star)Ole Gunnar Solskjaer

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer 

Arsenal itawasilisha ombi la kutaka kupunguziwa bei ya kumnunua beki wa kati na nyuma wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 20, kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi cha Unai Emery. (Sun)

Monaco wana nafasi ya kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 31, anayewachezea kwa mkopo huku tetesi zikisema kwa ada hiyo ni robo ya £29m iliyolipwa mwaka 2016. (Sky Sports)Islam Slimani

Real Madrid imemtambua kipa wa Athletic Bilbao Mhispania Unai Simon, 22, kama mchezaji ambaye huenda akachukua nafasi ya kipa wao wa sasa Mbelgiji Thibaut Courtois, 27. (El Desmarque, via AS)

 

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amemtaja Harry Kane wa Tottenham kama mshambuliaji mahiri lakini amekiri kuwa haoni kama klabu yake itafanikiwa kumhamisha nyota huyo wa miaka 26 kutoka London kaskazini. (Evening Standard)England's Harry Kane

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema angelipendelea kumsajili Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye mkataba wake katika klabu ya LA Galaxy unakamilika mwezi Januari. (ESPN)

Brendan Rodgers amemwambia kiungo wa kati James Maddison kuwa Leicester ni mahali anapoweza “kujikuza” licha ya Manchester United kuonesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 22. (Leicester Mercury)James Maddison

James Maddison

Juventus inafanya mazungumzo na Mario Mandzukic kuhusu uhamisho wake kutoka klabu hiyo mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Croatia wa miaka 33 amekuwa akilengwa na Manchester United. (Mirror)

Vilabu vya Derby, Huddersfield na Swansea vinamfuatilia mchezaji wa safu ya kati wa Fleetwood Kyle Dempsey, 24. (Football Insider)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents