Habari

Ole Sendeka apendekeza kuchunguzwa kwa akaunti za benki za wenyeviti wa kamati za bunge

Msemaji wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Christopher Ole Sendeka, ameitaka serikali kuwasiliana na Ofisi za Bunge ili kuchunguza akaunti za wenyeviti wa kamati za bunge hilo ambao maeneo waliyokuwa wanafuatilia yamebainika kuwa na ufisadi.

01

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Sendeka amesema, “Hivi chuki ya Zitto kwa serikali ya awamu ya tano inayopambana na mafisadi akiendelea kuinyooshea kidole kila kukicha wakati yeye alikuwa anasimamia mashirika hayo ambayo miongoni mwa taasisi hizo ambazo alikuwa anasimamia na baadhi ya marafiki zake ndio ambao wamenunua hekari 1 kwa milioni 800.”

“Kumbe walikuwa wanajificha nyuma ya pazia, kulikuwa na maslahi binafsi. Nadhani wakati umefika kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi si tu kuwashughulikia maafisa mashuhuri wanaoongoza taasisi hizo bali hata kuangalia akaunti za kamati za bunge na za viongozi wa kamati hizo waliokuwa wakizisimamia. Mashirika haya ambayo yameonyesha ufisadi mkubwa kuona kama akaunti hizo za kwao na maisha yao na mali walizonazo zinafanana na hizo walizokuwa wakilipwa kutokana na mapato yao halali,”ameongeza.

“Nilikuwa naangalia msukumo huu wa ghafla, mapenzi ya ghafla ambayo wengine wanajidai wanayapata kwa nchi hii kumbe ilikuwa ni kichaka kwa baadhi ya maswahiba wao wasichukuliwe hatua. Nataka niwahakikishie serikali ya Magufuli haina gia ya kurudi nyuma katika hili, tutasonga mbele tukijua dhahiri kwamba serikali ya watu iliyochaguliwa na watu inayowatumikia watu haiwezi kufutika duniani.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents