Habari

Ole Sendeka aunga mkono utafiti wa Twaweza

Msemaji wa chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka amesema amekubaliana na utafiti wa Twaweza kwakuwa watanzania wengi wana imani na kuupenda utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

twaweza-colour-logo

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa utafiti huo, ambapo alikuwa mmoja wa viongozi waliohudhuria. Utafiti huo uliopewa jina la Sauti za Wananchi, ulihusisha wananchi wa chama tawala, na vyama pinzani.

“Mmesikia ukwepaji kodi ambao ulikuwepo, kulikuwa na mtandao wa kuibia nchi uliokithiri na ambao kwa kiasi kikubwa naomba nikiri na kusema kwa miaka kumi ya uwakilishi wangu ndani bunge, yapo mambo mengi ya msingi yaliyokuwa yakihusiana na ustawi wa nchi yetu, kuna vitendo vya ovyo vilivyokuwa vikifanyika ambapo tulisimama tukasema haya yasitendwe,” alisema Sendeka.

Utafiti huo uliojikita katika suala la demokrasia, ulishirikisha wananchi 1602 kutoka Tanzania bara pekee.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents