Michezo

Olimpiki: David Rudisha wa Kenya ashinda medali ya dhahabu kwenya riadha

Mwanariadha kutoka nchini Kenya, David Rudisha amefanikiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki ya mita 800 kwa kutumia muda wa 1:45.09.

5568

Rudisha amekuwa mwanariadha wa pili kutoka nchini Kenya kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano hayo yanayoendelea huko nchini Brazil. Siku ya jumapili mwanadada Jemima Jelagat Sumgong kutoka Kenya alifanikiwa kushinda medali yake ya kwanza katika mbio za marathon upande wa wanawake.

Hii ni mara ya kwanza kutokea mwanariadha mmoja kushinda mbio hizo katika mashindano mawili mfululizo tangu 1964. Aidha Rudisha alifanikiwa kushinda medali hiyo ya dhahabu ya Olimpiki kwa mara ya kwanza Agosti 9, 2012 iliyofanyika nchini Uingereza baada ya kutumia muda wa 1:40.91.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents