Oliver Mtukudzi: Hakuna mtoto anayetakiwa kuzaliwa akiwa na HIV leo

Jumanne na Jumatano ya wiki hii mwanamuziki wa Zimbabwe Oliver Mtukudzi alifanya ziara nchini Tanzania.

Tofauti na ziara zake zilizopita ambazo zilikuwa za muziki zaidi, wiki hii amekuja kama balozi mwema wa Unicef ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini katika jitihada za kukuza uelewa kuhusiana na virusi vya Ukimwi na namna ya kumlinda mtoto.

Pamoja na kutembelea maeneo kadhaa, Mtukudzi alipewa muda wa kuandika masuala mbalimbali kuhusu Ukimwi kupitia akaunti ya Twitter ya Unicef Tanzania. Haya ni baadhi ya mambo aliyoyaandika:

“Hakuna mtoto anayetakiwa kuzaliwa akiwa na HIV leo. Inawezakana kuwalinda watoto wetu dhidi ya gonjwa hili.”

“Akina mama wote na wenzi wao wanatakiwa kupima HIV. Tambua afya yako ili upate matibabu.”

“Natumia muziki kuwapa watu matumaini, kuelimisha, kufundisha nidhamu binafsi na kuiponya mioyo iliyovunjika.”

“Ushiriki wa watoto ni ufunguo. Wazazi wanahitaji kuwasikiliza watoto wao. Mtambue vema mwanao na wasaidie.”

“Vijana wanatakiwa kupima, kuwa na mwenzi mmoja na kutumia condom kujikinga na HIV.”

“Tunahitaji kubadilisha mitazamo yetu. Tunahitaji kusisitiza upimaji wa HIV. Inawezekana kuwa na kizazi kisichokuwa na HIV.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents