Burudani

Ombi hili la Akon lakataliwa na serikali ya Marekani

Msanii wa muziki kutoka Marekani mwenye asili ya Senegal, AKON ombi lake la kutaka kusaidia kurejesha umeme katika visiwa vya Puerto Rico limekataliwa na serikali ya Marekani.

Tokeo la picha la akon
AKON

Akon siku ya Ijumaa ya wiki hii akiwa kwenye kiwanja cha ndege cha mjini Los Angeles, akihojiwa na mtandao wa TMZ alisema kuwa anashangaa kwanini mpaka sasa wakazi wa visiwa vya Puerto Rico bado wapo gizani.

Soma na hii – Pitbull atumia ndege yake kuokoa wahanga wa Puerto Rico

Alisema kupitia mradi wake wa AKON LIGHTING AFRICA angeweza kurejesha umeme pia kwenye kisiwa hicho kilichoharibiwa vibaya na kimbunga mwaka jana.

Akon amesema aliuambia mtandao wa TMZ kuwa bado serikali ya Marekani haijachelewa kupokea ombi lake kwani yupo tayari kuisaidia.

Serikali ya Marekani kupitia kwa msemaji wa White House, Sarah Sanders amesema kuwa ombi hilo limekataliwa kwani tayari bajeti ya kurejesha umeme visiwani humo imeshapitishwa kilichobaki ni utekelezwaji tu.

Mwaka jana mwezi Septemba maelfu ya watu katika visiwa vya Puerto Rico, walikosa huduma za kijamii baada ya visiwa hivyo kukumbwa na kimbunga Maria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents