Burudani

Ombi la Ray C kwa Rais Dkt. Magufuli, ni kuhusu wanawake kuolewa

Msanii wa muziki Bongo, Ray C ametoa ombi kwa Rais Dkt. John Magufuli kuhusu wanawake kuolewa.

Muimbaji huyo amependekeza kuwa kusiwepo na mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume hadi ndoa ili wanawake wengi waweze kuolewa. Kupitia Instagram yake ameandika;

Mzee mi na shida Moja! hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji Sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili!Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano ya Kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa!

Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila Cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea!Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe! Utakuwa umewanyoosha kisawasawa hawa Wanaume zetu Tutaheshimiana!
#NilivyoamkaLeo

July mwaka jana Ray C alikaririwa na kipindi cha FNL cha EATV akisema hayupo katika mahusiano na mtu yeyote kwani ameshapoteza muda katika mambo hayo hivyo hawezi kumpatia mtu nafasi hiyo tena kwani akili yake kwa sasa ameielekeza kwenye kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents