Burudani

OMG wafanya kolabo na msanii mkubwa Marekani

Kundi la muziki wa Bongo Flava, OMG limefunguka kufanya kolabo na msanii mkubwa kutoka nchini Marekani.

Member wa kundi hilo Con Boi ameiambia Ladha 3600 ya E Fm kuwa bado ni mapema kuweka wazi jina la msanii huyo ila ni kitu ambacho kimeshafanyika.

“Tumefanya kolabo nyingi sana nje ya nchi, watu wa duniani kabisa huko, tumefanya nao. Mapema sana itakuwa sio surprise tena, inabidi kazi zikitoka kuwe na uzito ili kutengeneza ule uzito inabidi vitu viwe vya kushtukiza,” amesema.

OMG kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma ‘Wanangu Na Wanao’ ambayo wamemshirikisha Rosa Ree.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents