Burudani

Ommy Dimpoz aeleza alichojifunza baada ya kuhudhuria show ya Beyonce and Jay Z, London

Hit maker wa ‘Tupogo’ Ommy Dimpoz amesema baada ya kuhudhuria show ya Beyonce and Jay Z jijini London, Uingereza amejifunza mambo mengi yatayokuja kumsaidia katika show zake nchini.

Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz aki shoot video yake London

Show ya hiyo aliyohudhuria, ilifanyika usiku wa April 28 jijini humo kwenye uwanja wa 02 Arena.

“Sijaenda kwenye show ya Beyonce and Jay Z kushangaa wasanii au nataka kumuona no,” Ommy ameiambia Bongo5. “Mimi nipo kwenye kujifunza zaidi ,nimejifunza kwamba kitu gani ambacho natakiwa kukifanya, endapo opportunity itakapo tokea. Mimi nimeangalia hata show zinazofanyika Channel O,ni tofauti na show zinazofanyika nyumabani. Sisi tunazungumzia production hata mimi plan yangu nitakavyokuwa nakuja kufanya show zangu basi nafanya show. Kama napata sponsor namwambia kabisa show yangu mimi nimeplan iwe hivi na hivi, lazima ukitoka hapo utengeneze story na jinsi utakavyoifanya ni rahisi ukitaka Hata kushoot unauza ile CD kwasababu standard yake itaonekana ina ubora,” ameongeza.

“Kuna vitu ambavyo nimejifunza hata kama kwa bajeti zetu ndogo wasanii pia wafanyabiashara, ukishaingia pale ndani utakuta kuna product za wasanii zinauzwa pale ndani, kofia,T-Shirt na nini ambavyo tu pale wanatengeneza hela nyingi sana ambacho kitu hicho kinawezekana hata kwetu sisi. Unaweza kuweka CD zako na nguo. Kwahiyo kama una product zako unazoziuza kwa kutumia brand yako ndio kitu ambacho kinaweza kukuingizia kipato cha ziada.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents