Burudani

Ommy Dimpoz aelezea kosa alilofanya hadi kuzuiliwa uwanja wa ndege wa Marekani na kurudishwa Tanzania

Muimbaji wa ‘Ndagushima’ Ommy Dimpoz, weekend iliyopita alizuiliwa uwanja wa ndege wa Marekani, na kurudishwa Tanzania hivyo kushindwa kufika kwenye show aliyotakiwa kufanya Las Vegas weekend hiyo.

Ommy D
Ommy alipokuwa kwenye ndege akielekea Marekani weekend iliyopita

Dimpoz ameelezea mkasa mzima ulivyokuwa hadi kurudishwa nyumbani licha ya kuwa tayari alikuwa ametua Marekani.

“Kilichotokea ni kwamba mi nilitoka hapa nikaenda mpaka Amsterdam, na Amsterdam nilikuwa naunganisha ndege kutoka Amsterdam kwenda Detroit na Detroit kwenda Vegas. Aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm. “Kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss flight ya connection ya kutoka Amsterdam kwenda Detroit ikabidi ni rebook booking yangu ili nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas.
Kwahiyo nikakosa ile connection ya kwenda Detroit ikabidi nipate connection nyingine kupitia Minnesota, nilivyofika kule ndege ambayo nilikuwa nimepata na connection niliyokuwa nimepata hii ya pili ikawa tayari imeshanichelewesha kwasababu nilitakiwa nifike usiku wa ile siku ya show, kwahiyo nikawa nimechelewa tayari, nikafika the next day.”

Aliendelea,

“Pale sasa kukawa kuna tatizo kule ikabidi wale watu wa siku ambayo walikuwa wameongea nao ilikuwa ni siku nyingine ikabidi waongee na jamaa kuwa jamaa amechelewa lakini tunaomba tufanye event next day, lakini jamaa wale wakakataa, na lengo ilikuwa mimi niperform kwenye hiyo weekend ya Rugby ile kama ulisikia alikuwepo Gyptian, Sauti Sol kwahiyo ilikuwa na mimi.”

Baada ya kufika uwanja wa ndege Marekani:

“Kwahiyo wakapiga simu (Uhamiaji) kule kwa wale watu wa event pamoja na venue, watu wa venue wakawaambia kulitakiwa kuwe na show hapa lakini msanii hakufika kwahiyo ikabidi waongee na promoter , promoters wakasema yah show tumeisogeza kwasababu msanii alichelewa alimiss flight. Sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo lilikuwa ni kwenda kwenye hiyo show na show tayari umeishai miss […] akasema kwamba lakini hapa unaonekana una show nyingine New York tarehe 21 nikawaambia ndio ilikuwa nikitoka Vegas naenda New York, wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusiasha chama cha kisiasa, na hata kama uliona kwenye promotion yangu ilikuwa nimeandika nitakuwa na show kwenye miaka 38 ya CCM Marekani […] kwahiyo wakaniambia kwamba hii Visa yako haikuruhusu wewe kuna aina ya visa nyingine ambayo unatakiwa uwe nayo ndo unaweza kuruhusiwa kuperform kwenye hiyo show.“

“Kwahiyo kwa kuangalia wakasema option iliyopo ni kwamba unatakiwa urudi nyumbani kwasababu shughuli ambayo ilikuleta imeshashindikana[…] Nikawaambia basi sawa mi nitarudi nyumbani, kwahiyo nasubiria tu sasa hivi promoter wale ambao waliandaa show ya Vegas wapange tarehe kwaajili ya hiyo venue ya show nyingine then ntaendelea na mchakato.”

Kwanini alichelewa ndege ya kuunganisha?

“Unajua nilishazoea kukaa zile connection za masaa matatu reporting time, kwahiyo pale nilijichanganya kwenye masaa […] kwahiyo katika kuangalia pale fikra zangu na mawazo nilishagazoea labda nimeunganisha kwenda D.C za kwenda L.A unakuta ukiunganisha unaweza ukakaa pale masaa matatu kufanya connection ya kwenda, lakini ile ilikuwa ni connection ya muda mfupi ni kama ya lisaa limoja kwahiyo mpaka ushuke utoke uende geti unalotakiwa kwenda, kwahiyo katika zile mishe mishe nikajikuta ile ndege mlango ishafungwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents