Ommy Dimpoz amwaga mahela kutengeneza video Afrika Kusini

[youtube]http://youtu.be/fjRYKAKZTNo[/youtube] Msanii wa hit ya ‘Baadaye’ Ommy Dimpoz alikuwa nchini Afrika Kusini ambako amefanya video ya wimbo wake huo.
Ommy alisafiri na muongozaji wa kampuni ya Visual Lab: Nect Level Adam Juma.
Shooting ya video hiyo tayari imeshakamilika na Adam amesambaza video ya jinsi mambo yalivyokuwa katika uchukuaji wa matukio ya kwenye video hiyo aliyoipa jina la ‘The Making of Baadaye’.
Kwa mujibu wa East Afrika Radio Adam amesharudi Tanzania tayari kwa editing ya video hiyo lakini haikusema kama Ommy pia amerudi.
Ommy alisema wameshoot kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.
Alisema location za kufanyia video nchini Afrika Kusini ni nyingi na watu wanajua umuhimu wa video ya muziki kufanyika kwenye location zao kuliko Tanzania.
Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton ambapo ameoneka model mmoja aliyewahi kuonekana kwenye video za wasanii wakubwa nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents