Burudani

Ommy Dimpoz atoa ujumbe mzito siku yake ya kuzaliwa ‘tusiishi kwa chuki na uadui’

Alhamisi hii 13th September ni siku ya kuzaliwa ya mwanamuziki Ommy Dimpoz ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini Tanzania.

Muimbaji huyo ambaye upo chini ya RockStar 40000, ameitumia siku yake hiyo kuandika ujumbe mzito kuhusu alichopitia kwenye maisha yake baada ya kupata matatizo katika mfuno wake wa kumeza chakula na kusababisha kufanyiwa upasuaji mkubwa nchini Afrika Kusini.

Ommy kupitia Instagram yake ameandika, “Leo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa.Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history.
Nilichojifunza kipindi hichi chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mitandao ila nia yangu ni kujaribu kukumbushana sisi kama Binadamu kuwa kuna leo na kesho kwahiyo tusiishi kwa chuki na Uadui maana hatujui kesho yetu itakuwaje!! Kuna kipindi wakati nimelazwa nilikata tamaa ya kuishi nikaona labda muda wangu umekwisha lakini hapo Hospital akaletwa mgonjwa mwingine ambae alikuwa pembeni yangu alishambuliwa na majambazi kwa risasi tisa mwilini lakini madaktari wakafanikiwa kuokoa maisha yake na akapona so nikajiuliza mimi ni nani nikate tamaa ya kuishi na nikajifunza kwamba kuugua sio kufa, Ni vyema tukipata nafasi basi tuwaombee na kuwafariji wagonjwa kwani wanayoyapitia ni magumu mno. Kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri na bado niko kwenye recovering, pia nawashukuru watu wote ambao mmekuwa mkiniombea dua nipone kwa haraka kuanzia mashabiki mpaka wasanii wenzangu na kila mtu aliyeniombea kwa imani yake Nashukuru sana. Mungu awabariki sana.
:
Pia Shukran za dhati kwa Familia yangu, Marafiki zangu wa Karibu, Management yangu ROCKSTAR FAMILY @officialalikiba na my lovely Manager @sevenmosha ambaye amehangaika na mimi mfano wa Mama Mzazi na mtoto wake pamoja na my Big Brother Governor @joho_001 ambaye ameniuguza kwa kipindi hichi chote chini ya uangalizi wake na Madaktari kuanzia Kenya Mpaka South Africa.
ASANTENI SANA NA INSHAALLAAH KWA UWEZO WA ALLAAH I WILL COME BACK STRONGER 💪🏽🙏❤

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents