Burudani

Ommy Dimpoz atoboa siri ya kukaa muda mrefu Uarabuni

Baada ya tetesi zilizovuma karibia mwezi wote wa Marchi mwaka huu kuwa Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz anakula bata Dubai kwa pesa za kupewa na Tajiri mmoja hapa Nchini, hatimaye msanii huyo anaetamba na ngoma yake ya Cheche amefunguka A-Z siri ya yeye kukaa Dubai kwa kipindi kirefu.

Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz amesema wakati anafika Dubai akitokea Marekani ambako alikuwa na AliKiba mwezi wa Marchi aliposti picha kwenye mtandao wa Instagram mapema alivyotua Dubai na kuweka Hashtag ya #HelloDubai hapo ndipo dili lilipoanza kwani alianza kutafutwa na Bodi ya Utalii ya Dubai kwa lengo la kufanya nae kazi.

Picha aliyoposti Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz amesema alitumiwa E-mail na Bodi ya Utalii ya Dubai wakimtaka kuongeza siku za kukaa Dubai kutoka siku tatu ambazo alipanga mpaka mwezi mmoja huku akitembezwa maeneo yote muhimu ya Utalii ndani ya Dubai na kupigwa picha na kuposti kwenye mtandao wake wa Instagram.

Kwa maelezo ya Ommy Dimpoz amesema likes na Komenti nyingi zilizotolewa kwenye picha hiyo ziliwaogopesha watu wa Bodi ya Utalii mpaka kutamani kufanya nae kazi.

Wakati natoka Marekani kwenye Tour ya Ali nilipofika Dubai nilipiga picha  na kuweka Hashtag ya #HelloDubai ambayo ilipata likes kibao so bodi ya utalii ikaona ile Hashtag na wakanitumia Email wakitaka kufanya kazi na mimi“,amesema Ommy Dimpoz kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Ommy Dimpoz amesema Bodi hiyo ilimtaka atembezwe kwa helkopita kwenye maeneo muhimu ya Dubai na kuposti picha akiambatanisha na Hashtag ya #VisitDabai ikabidi aingie mkataba nao wa kibiashara uliomuweka kwa mwezi mmoja Dubai.

Hata hivyo, Ommy Dimpoz ameishauri Serikali kutumia wasanii wa ndani kuweza kuitangaza nchi yetu kimataifa kwani wana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Unajua watu wengi huwa wanapenda kujaji maisha kwenye picha mimi napenda hata kuishauri Serikali yetu kufikiria mara mbili suala la kuwatumia Wasanii wa ndani kuitangaza nchi kwenye sekta ya utalii kwani wana followers wengi,“amesema Ommy Dimpoz.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents