Burudani

Ommy Dimpoz awachana wanaotumia umaarufu vibaya

By  | 

Msanii Bongo Flava, Ommy Dimpoz amewachana wasanii wanaopata umaarufu na kuutumia vibaya.

Akiongea katika kipindi cha Bongo Flava Top 20 cha East Africa Radio, mkali ambaye amesainiwa lebo ya Rock star 4000, siku chache zilizopita amedai kuwa wasanii wengi wanatumia umaarufu vibaya.

“Wasanii wengi bongo wanatumia umaarufu wao kufanya makosa mbalimbali katika jamii,” amesema Ommy.

Pia mkali huyo hakusita kuongelea swala la kudharau wimbo wa kunandikiwa ambao baadae akipewe mtu mwingine unakuwa mkubwa, vile vile amehaidi kuwa wiki ijayo anategema kuachia kichupa cha ‘Cheche’.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments