Burudani

Ommy Dimpoz: Hata kama Wema alikuwa katika mahusiano na D, haiwezi kunizuia mimi…Atolea maelezo picha zilizozua maswali

Ommy Dimpoz amevunja ukimya na kuzungumzia picha za yeye na Wema zilizoibua hisia kuwa huenda ameanzisha uhusiano na ex wa rafiki yake Diamond Platnumz.

Wema na Ommy

Picha za Ommy Dimpoz na Wema Sepetu zimezua maswali mbalimbali, wengine wakihoji kama ni sawa kwa mtu kuanzisha uhusiano na aliyekuwa mpenzi wa rafiki yake wa karibu.

Akizungumza kupitia Amplifaya ya Clouds Fm, Ommy ambaye amesema yuko Afrika kusini kwenye matembezi binafsi na Wema na washkaji wengine, ametolea maelezo picha hizo na uhusiano kati yake na Wema.

ommy na wema

“Ni picha tu mi naona kama picha zingine tu za kawaida nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana story Sio mara ya kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tuna picha nyingi sana ambazo tumepiga tangia tumeanza kufahamiana…”

10953376_1045282048819620_3651501053188108847_n

Aliendelea,

“Nafikiri zilizotengeneza story zaidi ni hizi ambazo zimeonekana kama tuko chumbani, kwasababu mi nilikuwa nimelala kiukweli tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja kwahiyo nilishtukia picha ziko kwenye mitandao. Unajua mnavyokaa kwenye apartment, kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washkaji wengine wengi wengi kidogo South Afrika…mnavyokaa kama familia kuna mambo ya utani utani, nikashtukia tu na picha zimetapakaa, kwahiyo ndo maana hata watu wakiniuliza nasema muulizeni Wema aliyepiga picha kwasababu mi nilikuwa nimelala kwahiyo sielewi zimepigwaje hizo picha.”

“Kuhusu labda mimi kufahamiana na Wema nimefahamiana naye siku nyingi hali kadhalika D, ushikaji wetu hao watu wote nimekuwa nao karibu kipindi tofauti kabla hata pia hawajawa katika mahusiano mimi tayari ni watu wangu before hawajawa kwenye mahusiano yao ya kimapenzi, kwahiyo sidhani kama hapo kuna big deal au mimi kuanza kuwaelezea oh nilikuwa sijui na Wema tulikuwa labda sehemu hivi na hivi kwasababu ni mshkaji wangu tangia siku nyingi hata kama alikuwa katika mahusiano na D, yakatokea mahusiano yao pengine hayako sasa hivi haiwezi kunizuia kunifanya mimi niharibu ushkaji wangu, yaani kwasababu hivyo ni vitu vyao binafsi wao.” Alimaliza Ommy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents