Burudani
Ommy Dimpoz leo awasili London kuungana na Ali Kiba kwenye ziara yao ya Valentine
Hitmaker wa Me and You, Omary Nyembo aka Ommy Dimpoz leo amewasili jijini London Uingereza kujumuika na Ali Kiba aliyekuwepo huko kabla yake, kwaajili ya ziara iliyopewa jina la The Valentine Tour.
Promota wa ziara hiyo Victor Djrule wa kampuni ya Bongo UK amepost picha za Ommy Dimpoz baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa London Heathrow Airport (LHR) ambapo Ali Kiba alikuwepo pia kumpokea.
Wakali hao wa Bongo Flava watakuwa na show Feb 22 na 23.