Omotola Jalade: Mwanzoni sikuwa nampenda mume wangu



Muigizaji maarufu wa kike nchini Nigeria Omotola Jalade-Ekeinde ambaye mwezi uliopita alitua nchini kumpa support Wema Sepetu kwenye uzinduzi wa filamu yake Superstar, yupo kwenye ndoa kwa miaka 16 sasa.
Lakini haikuwa rahisi mwanzoni. Ukweli ni kwamba alikuwa hamzimii mume wake.
Akiongea na mtandao wa nigeriafilms.com mrembo huyo amesema: “Siku zote huwa nawaambia watu kuwa nilipokutana naye, sikuwa nampenda lakini yeye alisema ‘it was love at first sight’ hivyo nimejifunza kumpenda. Nilivutiwa na yeye sababu ya ukomavu wake (maturity). Niliona uwezo wake wa kuniona mimi. Namaanisha kuwa ananijua kuliko hata mimi ninavyojijua. It is just weird I can’t explain. You just can’t get it. But he feels my pain, it is easy for him,” alisema.
Muigizaji huyo na mume wake wana watoto wane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents