Burudani ya Michezo Live

On Her Birthday: Exclusive Interview na Wema Sepetu kuhusu maisha yake, Kanumba, Diamond na mengine

Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28 September hivyo leo ni birthday yake. Taja wasichana wote wa Bongo Movies wanaotamba Tanzania, usipoliweka jina la Wema Sepetu orodha haijakamilika. Wema Sepetu ni supastaa asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na websites/blogs. Mfahamu zaidi kwa undani leo anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa katika mahojiano haya aliyoyafanya na Bongo5 kwaajili ya jarida la Mzuka.

_DSC1063 copy

Kwenu mko wangapi na wewe ndio mtoto wa mwisho?

Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu. Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana familia yake. Wa kwanza yuko kule anafanya kazi ana mtoto mmoja. Wa tatu yuko kule anasoma na anafanya kazi

Miaka mitano kabla ya mwaka 2006, Wema alikuwa ni msichana wa aina gani?

Wema alikuwa ni msichana wa kawaida. Wakati ule ulikuwa ukiniuliza unataka kuwa nani ukikua ningekujibu nataka kuwa air hostess sababu dreams zangu zilikuwa ni kuwa air hostess, sijawahi kufikiria kabisa kuingia kwenye fame. Though nilikuwa nawaangalia watu kama Ray C, K-Lynn, Kwasababu mimi nilikuwa nasoma academic na shuleni kwetu nakumbuka tulikuwa tukitoka ile home time kulikuwa na duka fulani hivi la mpemba tunaenda tunakula sambusa nini, so magari yatapita nini and we would see Ray C and everybody will go like ‘you see Ray C’ you know, kwahiyo we go crazy over superstars na watu famous.

Kiukweli I never so myself kuwa katika this position ambayo niko. Kwahiyo nilikuwa tu msichana ambaye sina ndoto za kuwa star lakini nilikuwa tu nawashangaa masupastaa. My dad amekuwa anapenda sana mashindano ya Miss Tanzania and kila mwaka alikuwa anamake sure kwamba amenunua tiketi ya kwenda kuangalia Miss Tanzania.

So nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa akina Sylvia Bahame tumekaa nyumbani amekosa tiketi. Akakaa akasema ‘kumbe ukiwa umekaa nyumbani ndio unaenjoy vizuri kuliko hata kwenda pale’ akasema ‘one day nawish one of my beauties hata kama hatoshinda, nikilipia tiketi naenda nikijua kabisa nimeenda kumlipia binti yangu.

So sikukiweka kichwani hicho kitu lakini after kuingia katika whatever na nini, so siku nimekaa na dad nikamwambia ‘dad unakumbuka kuna siku ulisema hivi’ akasema ‘yes I remember’ . Hata Mange Kimambi alivyokuja kuniapproach, alivyoniona Sleep Way akaniambia kwamba anataka niingie katika mashindano, nikamwambia kwamba mimi nina wazazi wangu, siwezi nikaamua tu mimi mwenyewe na mimi nakaa na wazazi, so nilivyoongea na mama akasema ‘ongea na baba yako’ nikampigia simu baba alikuwa kipindi hicho Dodoma, akaniambia ‘fanya my beauty nitakusupport’, hakuthink twice alinipa go ahead kabisa.

Kabla ya Miss Tanzania, ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu Wema Sepetu, ni vipi Miss Tanzania ilibadilisha maisha yako hasa kutokana na watu kuanza kufuatilia maisha yako na chochote unachofanya?

Ni kitu ambacho nilikipata bado nina umri mdogo and nilikuwa sijajiandaa, nilikuwa naichukulia tu poa this whole issue ya kuwa kwenye spotlight. Nilikuwa sidhani kama itakuwa vile kwasababu kama wanavyosema experience ni bora uexperience mwenyewe usione kwa wenzako so nilivyokuwa naichukulia ni tofauti na ilivyokuja kuwa kwasababu mimi nilikuwa naichukulia tu ‘kuwa star raha’ umeenda watu wamekushangaa nini lakini nilivyokuwa nimeingia sana katika ile spotlight nikasema kumbe ooh my God it’s this hard.

Kwahiyo ikawa ni kitu kilichonipa wakati mgumu sana kukizoea like mpaka sasa hivi naweza kusema kwamba ile umetoka kila mtu kakuangalia nini, it’s not an easy task, yaani haizoeleki hiyo hali yaani kila siku unazidi kuiona mpya kwasababu there is no place unaweza ukaenda ukawa na privacy yako, yaani upende usipende lazima utakuwa ni attention kwa watu, lazima watu watakuangalia. Sometimes natamani tu na mimi niwe Wema lakini huwezi sababu all eyes on you. And a lot of times as a normal human being kuna time unahisi you just be yourself lakini inakuwa ni time chache chache sana. The only place where I can be myself is in my room and in my house, out of my gate you cannot be yourself.

Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?

Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba mwenyezi Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio amenipangia hivi nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa kila mtu, lakini siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda mara moja mara mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi ukapata regrets kama hakuna tatizo.

Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa Miss Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa na pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha hayo ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?

Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani lakini hatushei sana zile common interests kama zamani because once upon a time tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo kwenye spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao naonana nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being Miss Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja.

Ulikuwa na boyfriend tayari?

Yes nilikuwa naye

Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?

Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza kusema. Sana sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend ambaye unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia ‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya kwamba sishiriki.

So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha yangu kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti kuanzia naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye gazeti. So kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ so sikuonana naye the whole day.

Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa namsikiliza. Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’. Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho tunaongea, tunasalimiana’

_DSC1055 copy

Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?

Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada yangu.

Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana protective kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya pale nyumbani kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different furnitures, so tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la Mwanamboka kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda pale wakati tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao nini ,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, tumepark gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya tukasalimiana akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na mimi napenda unavyoigiza’ nini na nini.

Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’.

Nikamwambia siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle Hashimu wataniua wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila kuwaconsult so akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati ananiambia tuachie nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja umemuona Wema?’ Aliniringia sana.

‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia poa,’Kaka basi chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza tukamtumia kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani. Basi nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza, ‘Hee Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao.

Basi, so baada ya hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep nikamsave, basi mimi nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba inanipigia ambayo nimeisave vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’ akaniambia ‘vipi, safi Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’ ‘haya basi sawa basi baadae’ nikamwambia ‘poa’.

Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext ‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi uko wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia ya kutextiana kila siku tunandelea for one weak tunatext mara yeye ataniuliza umekula nini, mara sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu unajua kwamba mwanaume akiwa ana interest na wewe. Kidogo tukaanza kuulizana una boyfriend una girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia mimi ‘nipo kambini Lamada’ akanielekeza nikafika.

Basi nimefika siku hiyo tumekaa pale garden akaniambia ananipenda na nini, hivyo. Kipindi hicho nilikuwa sina boyfriend nilikuwa very very single, so nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na boyfriend wangu sijui nini’ akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie basi’ Nakumbuka tulivyokuwa tunaondoka ndo tukakiss, it was our first kiss. Basi nikaondoka, akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia siwezi akaniambia please, please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia ‘sawa’ basi nikarudi then akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi yakaanza.

Basi kwenye mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact movies na wewe’ nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi unaweza kuact hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia ‘unaweza kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’ akaniambia ‘basi kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu ukimenya si unalia, basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ .

Akaniambia niende kuonana na bosi wake. Nilivyofika tu ofisini nikaonana na Mtitu Game. Akanipa script akaniambia nikasome kama story akaniambia ‘wakati unasoma uwe unasoma sana concentrate kwenye Dina. Basi vile tukiwa tukikutana tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa basi wewe you are ready to shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, hauwezi amini, I just felt yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa wengine wanaona it’s hard unajua.

Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back to school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka ya International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu ya Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona kwamba kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo soon naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’

Nimerudi kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White Maria yaani tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa nimeshajikuta katika movie, so that why I keep saying kwamba without him nisingejua.

_DSC1040 copy

Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika mahusiano yako yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?

Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu).

Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu.

Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda. So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.

Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia.

Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikumuuliza anakataa.

Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja.

_DSC1061 copy

Mwaka jana alipooenda kutumbuiza kwenye Big Brother Africa, alidai kuwa ameweza kuongea Kiingereza kwasababu yako, ulikuwa ukimfundisha ama ulikuwa ukipenda kumuongelesha Kiingereza zaidi?

Yes. Naseeb alikuwa hajui Kiingereza, alikuwa anajua cha juu juu. Ila mimi na Naseeb tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume. So mimi nilivyo kidogo nimetupia Kiingereza kwahiyo hiyo ilikuwa inampa tabu kwenye the first two months kwahiyo most of the times nikawa naongea naye Kiingereza. Lakini he is smart, Naseeb is very smart yaani akiwa haelewi kitu ‘hivi baby hapa kwenye has na have unafanya nini, hapa natumia tense gani? Niweke ing niweke nini?’ mwisho wa siku nikajikuta like tunatumia most of the time kufundishana. Akisema kitu ambacho sicho namwambia ‘usije ukarudia tena kusema hivyo mbele za watu watakucheka’. So akajikuta tu anaweza.

Kwanini mliachana?

Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate .Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.

Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu.

Unamiss chochote kutoka kwake?

Normally inakuaga ni ngumu sana kuadjust kwa maisha mapya. It’s always very hard kuanza tena love life sababu apart from mapenzi kuna kuna mazoea so inakuaga ngumu sana at the beginning. Nilikuwa, lakini not anymore sasa hivi naona kawaida tu kama tulivyoachana na wengine. Silook back nikamiss chochote, everybody is happy now.

Hivi majuzi yeye na mpenzi wake wa sasa Penny walikurekodi baada ya wewe kumpigia simu Diamond, ni kwa kiasi gani tukio hilo lilikuvunja moyo wako?

Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very disappointed.

Ni kweli lilisababisha utamani kufa ama kulikuwa na jambo jingine?

Maneno yalikuwa mengi sana halafu ilivyotokea nilijipa moyo, ‘you know what’ F it, bullshit ni mshenzi tu, mshamba tu ambaye hajaenda shule. Lakini kitu ambacho kilinifanya niwe torn ni the next day baada ya kuona post ambayo wanasema kwamba ni fake ya Diva, alitukana tukana sana, that was kitu kilichonifanya niwe like okay…… Lakini with the support and help ya watu ambao wananisurround, my family friends, the people who love me, wakanipa moyo.

Je! Ni sababu ya wewe kwenda vacation Arusha?

Yeah. My manager alinifanyia hivyo just to easy me up for whatever that imetokea.

Penny alikuwa rafiki yaki tangu utotoni, unahisi alikuzunguka kwa Diamond?

It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu.

Una nyumba yenye thamani ya milioni 400…

Sio shilingi milioni mia nne ni milioni 280. Milioni 400 watu wameniquote vibaya because Zamaradi aliniuliza ‘your empire ina worth kama shilingi ngapi’ ndio nikasema about… so nyumba no, niliinclude nyumba na magari na nini.

Okay, gaari karibu milioni 80, ofisi yenye thamani ya takriban milioni 70, uliwanunulia Gucci na Vanny vitu vyenye thamani ya karibu milioni 6, ulimtolea Kajala milioni 13 na mengine mengine, hivi how rich are you Wema? Are you a millionaire?

No, I’m just a normal person, not a millionaire, not a billionaire; I’m just Wema trying to live life.

Kwa mtanzania suala la kutumia mamilioni kwaajili ya shopping kwa mbwa tu haliwaingi akilini haraka, Vanny na Gucci wana thamani gani kwako mpaka uwagharamikie hivyo?

Vanny na Gucci are my everything. They are my everything because Wema Sepetu hana watoto, sina mtoto ila nawish kuwa na mtoto Inshallah mwenyezi Mungu akinijaalia nikapata uwezo wa kubear mtoto nitafurahi. Bado nadhani mpaka mwenyezi Mungu akinipa hiyo blessing ya kuwa na mtoto. Since then sina, so nawachukulia Vanny na Gucci kama watoto wangu, they are my babies. They are the reason mimi nikienda nyumbani niko stressed, they always make me smile. They are faithful, wako innocent; they are loyal hawawezi kunibetray, hawawezi kunihurt in anyway. Vanny akiumwa au Gucci nikimuona hayuko sawa I go crazy mpaka huwaga nalia. Tayari wana connection na mimi ambayo siwezi kuifananisha na kitu chochote. So they are my world. Kwahiyo mtu akitaka kumess na mimi amess na mbwa wangu hakutakalika I swear, I can do anything for those creatures, I can give my all for them.

Kitu gani ambacho ungependa watanzania wakifahamu kuhusu wewe ambacho unahisi wanapotoshwa?

The fact that wanavyosema mimi napenda scandal, mimi sipendi scandal , sipendi, hakuna binadamu anayependa scandal. I live to what makes me happy and kukifanya siogopi labda ndio kitu ambacho kinanicost. Naweza kusema kuwa kitendo cha mimi kuwavalisha nguo mbwa wangu kimewashangaza wengi lakini it makes me happy. If I look at them wako cute, wamependeza na sio nguo za binadamu zile ni nguo za mbwa kabisa ziko designed for dogs, ni viatu vya mbwa ambavyo viko designed for dogs, I can afford it, why not getting for my dogs, it makes me happy I live to it. Naweza kusema kwamba the fact ya mimi kuishi vile, roho yangu inapenda ndio inayonicost. Niko na mtu fulani, I want to make him be public kwa watu kwanini wasimjue, it makes me happy, I do it inanicost, ‘Wema Malaya sijui nini’ ndio kinachonicost.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW