Bongo5 ExclusivesMahojiano

On Her Birthday: Nancy Sumari ajibu maswali 10 muhimu (Exclusive Interview) Details+Audio

Siku kama ya leo miaka 27 iliyopita, Miss Tanzania 2005 na Miss World Africa, Nancy Sumari alizaliwa. Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, Zuri amefanya interview exclusive na Bongo5 kuhusu birthday yake.

993342_10151617972203380_833391356_n


Kuhusu kitu kikubwa anachoshukuru kwa mwaka aliopita

Ni mafanikio makubwa na blessings nyingi ambazo nimezipata. Kuwa na uwezo tu wa kuja kazini kila siku, kufanya kazi na timu ambayo imesimama kufanya kazi na wadau, sponsors, kuweza kuandika kitabu na kukipublish na kukisubmit wizarani, blessings ni nyingi sana. Ninapata support kubwa sana kutoka kwa familia yangu, rafiki zangu, yaani ni mtu ambaye nina mengi ya kumshukuru Mungu kwakweli.

Kuhusu kitu kikubwa anachokiona katika umri alionao sasa

Ni mabadiliko tu ya muonekano wa maisha. I think unavyoendelea kuwa mtu mzima vitu vinabadilika. Kwangu nyumbani ni muhimu zaidi kuliko sehemu yoyote nyingine. Siku za nyuma yaani kwenye ujana ikifika Ijumaa ni kitu cha kitaa. So sasa hivi vitu ambavyo naviona ni muhimu vimebadilika sana, I think ndio utu uzima huo, utu uzima dawa.

Kuhusu anachotazamia kufanya mwaka huu, kama mama, mwanafunzi na kama Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5

Katika kila Nyanja natarajia kufanya mabadiliko chanya kwenye jamii. Kama mama ningependa kumlea mtoto wangu kwenye maadili ambayo mimi naona yapo sahihi na pia kusukuma hiyo meseji kwa wazazi walio wengi zaidi, maybe kupitia blog yaani kushare experience zaidi na kujifunza pia kwa wazazi wenzangu ili kuiendeza jamii yetu ikue kwa maadili yaliyo joint, yanayoweza kuwaendeleza watoto wetu ili tuwaone wao in the future wanakuaje kutokana na malezi yetu sisi. Kama mwanafunzi, ofcourse ndio namalizia chuo kwahiyo niko very excited, Mungu amenisaidia naendelea kufanya vizuri.

Kama MD, kama ilivyo jadi yetu ni kuendelea kwenda mbele zaidi, kusukuma mipaka kwenye burudani, kwenye social entrepreneurship, kwenye entertainment, yaani kila nyanja ambayo tunaiguza. Tunataka tuwe mbele zaidi na tunataka tufike miaka 10 kabla ya wenzetu.

Kuhusu kumbukumbu nzuri zaidi ya birthday aliyonayo

Nadhani ilikuwa mwaka juzi ambapo ndio birthday yangu ya kwanza nilikuwa na mtoto wangu, nikawa na mwenzangu. Tulisherehekea kwa pamoja kama familia. That was the first birthday ambayo nilihisi my life is complete.

Kuhusu kama anategemea kufanya kitu kikubwa kwenye birthday yake leo

Sitegemei kufanya kitu kikubwa sana. Ni kutoa tu shukrani kwa friends, kusherehekea na family kidogo.

Kama amewahi kuchukia baada ya mtu wake wa muhimu kusahau birthday yake

Huwa hawasahau kwasababu ni wajanja kwa mfano leo nilitegemea wazazi wangu wangesahau, kaamka asubuhi mdogo wangu kawapigia simu, yaani kukumbushana so hawajawahi kuharibu na nawashukuru kwa hilo.

Kuhusu kama amewahi kuamka asubuhi na akasahau birthday yake hadi alipokumbushwa

I think wakati ule nipo boarding shule manaake kila siku zinafanana. So hiyo siku nimeamka nikawa nimesahau kabisa. Mawazo yote yapo kwenye issue nyingine tofauti sio birthday lakini after that haijawahi kutokea kwakweli kwasababu ni siku muhimu kwangu.

Kuhusu nani amekuwa mtu wa kwanza kumtakia birthday njema

Zuri na baba yake wamekuwa wa kwanza yaani tangu wiki iliyopita wameanza kuniwish happy birthday. Kwasababu alikuwa anajibu kumfundisha yaani Zuri aanze kuimba happy birthday so wao ndio walikuwa wa kwanza then friends ndio wakafuatia yaani watu wote ambao wananijali na mimi nawajali nadhani leo wamefikisha ujumbe so it’s very special.

945375_10151564424903380_108634874_n
Nancy na Zuri kwenye kava la jarida la Bang

Kuhusu kama ameweza kujibu wishes zote anazopata kwenye Twitter

Najitahidi nizijibu zote kwasababu nahisi mtu akiwa amechukua effort yake kukukumbuka akakuwish yaani ni furaha tu so najitahidi najibu zote.

Kuhusu anachotarajia kupata kwa dinner leo?

I think itakuwa something simple, something small. Mimi kawaida napenda vitu ambavyo viko small, simple yaani mnasherehekea lakini at the same time mnakuwa thankful.

Nyimbo tatu anazopenda kusikiliza leo

Naomba unichagulie Top 3 ya Marimba Music Chars ya wiki iliyopita.

Sikiliza Interview yote hapa.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/104380199″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents