Michezo

Operesheni Sanchez, Mourinho asisitiza kufunga mjadala na Arsenal baada ya kutua Old Trafford (+Picha)

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amewasili katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatano asubuhi huku ikiwa timu hiyo inakaribia kumsajili Alexis Sanchez.

Mourinho amewasili katika maeneo ya mazoezi ya Aon Training Complex wakati mazungumzo na Arsenal yakiendelea ya dau la paundi milioni 35 kunasa saini ya mchezaji wa kimataifa wa Chile, Sanchez.

 

Baadhi ya wacheza wa klabu hiyo wameonekana kuwasili makao makuu ya timu hiyo akiwemo Martial,ambaye alikuwa wakwanza kufunga bao siku ya Jumatatu usiku dhidi ya Stoke na kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0.

Marcus Rashford, Juan Mata, Scott McTominay, Daley Blind na Sergio Romero piia wameonekana kuwasili akiwemo na Mcameron, Borthwick-Jackson ambaye amerejea kutoka kwa mkopo Leeds United.

Marcus Rashford akiwasili Aon Training Complex

Anthony Martial akiendesha gari akiwasili Old Trafford baada ya kuisaidia timu yake mbele ya Stoke

Sergio Romero akiwasili makao makuu CarringtonĀ 

Mcameron, Borthwick-JacksonĀ  akiwasili baada ya kurejea kwa mkopo Leeds

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents