Burudani

Oprah amfuata Rihanna Barbados

Weekend hii Rihanna alipata mgeni maalum nchini mwake Barbados ambaye si mwingine zaidi ya Oprah Winfrey.

Baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya visiwa vya Carrebean, Rihanna alichukua fursa hiyo kumtembeza katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bridgetown kwa kutumia mkoko wake, Suzuki Jeep.

Rihanna pia alimpeleka Oprah kwenye makazi yao ya zamani. Oprah aliutumia mtandao wa Twitter kuwapasha habari followers wake kuhusiana na safari yake, “Look who’s driving me around Barbados!”, kukiwa na picha yake na Rihanna kwenye Jeep hiyo.

Oprah, 58, ameenda Barbados kufanya mahojiano mahsusi na Rihanna mwenye miaka 24 kwaajili ya show yake, Oprah’s Next Chapter.

Kipindi hicho kitaruka hewani August 19 kwenye kituo chake cha OWN.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents