Orodha mpya ya mafisadi yatua Ikulu

Waziri Mkuu PindaOrodha ya watumishi wa Serikali wanaotuhumiwa kushiriki katika tukio lililoiwezesha kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond kuingia mkataba wa kifisadi ulioiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya pesa imetua Ikulu

Orodha ya watumishi wa Serikali wanaotuhumiwa kushiriki katika tukio lililoiwezesha kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond kuingia mkataba wa kifisadi ulioiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya pesa imetua Ikulu kwa ajili ya kusubiri hatua za kiutawala kuchukuliwa dhidi yao.



Akisema na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Waziri Mkuu Bwana Mizengo Pinda amesema, mpaka hivi sasa tayari Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo ameshakabidhiwa orodha ya wahusika na kupewa maelekezo namna ya kuchukua hatua za kisheria na kiutawala.



Bw. Luhanjo anatakiwa kuchunguza na kuwachukulia hatua watumishi wote wa Serikali wanaotuhumiwa na sakata hilo la mkataba `bomu` wa Richmond, lililozua gumzo kubwa nchini.


Miongoni mwa watuhumiwa waliohusishwa na sakata hilo na kutakiwa kujiuzulu kutokana na kuzembea ama vinginevyo, ripoti ya Kamati hiyo ya Bunge ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Edward Hosea na Mkurugenzi wa Nishati na Madini katika Wizara ya Nishati na Madini Bw. Bashir Mlindoko.



Mapendekezo ya kamati hiyo teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Dk. Harrison Mwakyembe, kigogo mwingine anayepaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi.



Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda, watuhumiwa hao wanaweza kutimuliwa kazini au kupunguziwa madaraka, kutokana na uzito wa makosa yao au vinginevyo, kadiri sheria zitakavyoruhusu.



“Maelekezo yote amepewa Katibu Mkuu, suala hili sasa linafikia mwisho kwa kuwa anaandaa hatua za kuwachukulia, kama ni kuwafukuza kazi au kuwateremsha vyeo, well and good,“-Bw. Pinda.



Waziri Mkuu amesema hivi sasa Serikali haikubali kuchafuliwa na hivyo kila anayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi anawajibishwa


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents