Burudani

Orodha ya vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Afrika yatajwa, Tanzania yatoa vijana 8 ‘Diamond na Jokate watoswa’

Taasisi inayojishughulisha na tafiti mbalimbali zinazohusu vijana wenye ushawishi zaidi walio chini ya miaka 40Β  baraniΒ  Afrika ya The Africa Youth Awards, imetangaza orodha ya majina ya vijana 100 ya vijana wenye ushawishi kutoka kwenye mataifa 26 barani Afrika kwa mwaka 2018, na Tanzania ikiwemo.

Kutoka Tanzania, vijana waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo ni vijana 8 ambapo majina hayo ni Alikiba, Faraja Nyalandu, Herieth Paul, Jennifer Bash, Jumanne Mtambalike, Mbwana Samatta, Millard Ayo na Yusuf Bakhresa.

Kwa upande majina makubwa ambayo mwaka jana 2017 yalitangazwa kwenye orodha hiyo kama, Diamond Platnumz, Idris Sultan na Flaviana Matata mwaka huu yamepigwa chini.

Tazama orodha kamili hapa chini na kusoma zaidi kwenye website yaΒ The Africa Youth Awards.

Related Articles

24 Comments

  1. Uti unatumaliza kilichoongelewa ni ushawishi na mnatakiwa kujua ni ushawishi wa aina gan mm sina tim ila tukiacha upendeleo kwa mfano sisi ni watanzania tuna tamaduni zeti je kwa hao wanaosema mbona diamond hayupo kwa nn hiv mnadhan anayoyafanya yanaleta maadili gan kwa wanaomwangalia leo ameanza kuvaa vikuu mara kusuka nk hiv hapo anatushawishi nn kuiga mambo ambayo sio tamadun zetu au msinielewe vibaya ila washauri wa diamond wanampoteza na sisi mashabiki tutazidi kumpoteza kwa kumsifia japo ameharib

  2. Mzee James Mpashe huo utafiti wa mtu tu kafanya hata wewe unaweza kufanya ukatoa,imagine mtu Kama diamond hayupo hakat akifanya kitu kwa mda mfupi tuu vijana wa afrika mashariki wanajua na ni dhahiri kabisa ndie mwenye ushawishi mkubwa Afrika mashariki,kwaiyo izoo tafiti ni za kisenge mamaee

  3. Tanzania nzima vijana wengi wananyoa kama Diamond, wanavaa kama Diamond ,
    Sijawahi mtu anaye vaa kama Milad Ayo sijawahi kuona mtu kanyoa kama king Kiba ,so vitu vingine πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

  4. Sio vigezo vyao kunyoa na kuvaa peke ake. Wanaangalia mambo ya msingi na kimaendeleo. Unataka kuniambia hakuna wanawake wanaovaa kama faraja kota au kusuka kama faraja kota!? Fuatilia faraja kota anafanya mishe gani utajua kwanini yupo kwenye list. Millard anafanya kazi nzuri kila mtu anajua. Herieth paul ni msichana mdogo kafanya umodo kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa kuliko mamodo wenye miaka 20 na zaidi. Anyway pengine tunatofautiana uelewa sikulaumu

  5. Sio vigezo vyao kunyoa na kuvaa peke ake. Wanaangalia mambo ya msingi na kimaendeleo. Unataka kuniambia hakuna wanawake wanaovaa kama faraja kota au kusuka kama faraja kota!? Fuatilia faraja kota anafanya mishe gani utajua kwanini yupo kwenye list. Millard anafanya kazi nzuri kila mtu anajua. Herieth paul ni msichana mdogo kafanya umodo kwenye majukwaa makubwa ya kimataifa kuliko mamodo wenye miaka 20 na zaidi. Wanaangalia mambo ya kuwasaidia vijana na jamii kwa ujumla sio mambo ya kusutana au kuvaa vimodo

  6. Diamond ameshawishi wangapi kuingia kwenye game ? acheni mambo yenu
    kweli uelewa tunatofautiana kabisa .
    Eg:King Kiba ameshawishi nn ? sawa Faraja Kota kashawishi ndio najua …..
    Hem turudi nyuma walikuwa wanatafuta vigezo gani kwenye hivi vimatangazo vyao?

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents