Michezo

Oscar Pistorius apatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake

Mahakama ya rufaa ya nchini Afrika Kusini, Alhamis hii imempata Oscar Pistorius na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

1161338_965574

Jaji Eric Leach alitangaza kuwa rufaa ya serikali kwenye kesi ya Pistorius imefanikiwa. Jaji huyo ameirudisha kesi hiyo kwenye mahakama ya chini ili itoe hukumu mpya.

Pistorius, 29, alimpiga risasi girlfriend wake aliyekuwa na miaka 29 nyumbani Pretoria, February 14, 2013. Alidai kuwa alimpiga akidhania ni jambazi aliyevamia nyumbani kwake.

Baada ya uamuzi huo, June Steenkamp mama yake Reeva alimkumbatia rafiki yake Jenny Strydom kwa furaha.

Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano October mwaka jana na alitolewa baada ya mwaka mmoja kwenda kuendelea na kifungo cha nje.

Kwa uamuzi mpya, sasa mwanariadha huyo mlemavu atakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents