Michezo

Oscar Pistorius kutoka jela August mwaka huu

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini aliyehukumiwa kufungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Oscar Pistorius ataachiwa kutoka jela mwezi August, imeripotiwa.

Oscar-Pistorius

Pistorius alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana baada ya kupatikana na hatia za kumuua kwa risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake wakati wa Valentine’s Day mwaka 2013. Mwanariadha huyo alidai kuwa alimuua mpenzi wake kwa kudhania alikuwa jambazi.

Anaruhusiwa kutoka jela na kwenda kuendelea na kifungo cha nje ambako atakuwa nyumbani kwa uangalizi maalum mwezi August. Ndugu zake wamethibitisha kuwa wanatarajia Pistorius kuachiwa wiki chache zijazo.

Kwa mujibu wa ENCA News, Pistorius alikutana na bodi ya parole wiki iliyopita na tarehe ya yeye kutoka kupangwa kuwa August 21.

Familia ya Reeva Steenkamp imedai kusikitishwa na hatua hiyo na kusema kuwa kifungo cha miezi kumi kwa Pistorius hakitoshi kuwa adhabu kwa kosa alilofanya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents