Habari

OSHA yahitimisha kozi ya taifa ya Usalama na Afya mahala pa kazi, Washiriki 107 wanufaika (+Video)

Uhitaji wa mafunzo ya Usalama na Afya mahali pa kazi umeongezeka kwa kiwango cha juu hapa nchini jambo ambalo linaashiria kupanuka kwa uelewa wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi miongoni mwa watanzania.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, alipokuwa akihitimisha mafunzo ya Kozi ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambayo hutolewa na OSHA .

Mwenda Amesema kozi hiyo ambayo imetolewa kwa wiki tatu mfululizo katika Ofisi za OSHA zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, ilikuwa na jumla ya washiriki 107 kutoka katika taasisi, makampuni, mashirika na watu binafsi kutoka katika mikoa mbali mbali kote nchini.

Kwa upande wao washiriki wa Kozi hizo Bi. Hawa Said Mohamed, mshiriki wa mafunzo hayo amesema madunzo hayo ni mazuri na muhimu sana kwa watanzania wote katika kuimairisha masuala ya Afya na Usalama katika sehemu mbali mbali za kazi.”

Naye Mwita Jacob, ambae pia ni mhitimu wa kozi hiyo, alisema mafunzo hayo ni nyenzo muhimu katika kupunguza ajali, magonjwa na vifo vinavyoweza kusababishwa na mazingira hatarishi ya kazi kwani yanawaandaa wataalam kwaajili ya kuandaa na kusimamia mifumo ya kulinda Afya na Usalama wa wafanyakazi katika sehemu za kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents