Burudani

Otile Brown autangaza ujio wake mpya nje ya label yake Dreamland Music Empire

Baada ya mchakato ulioleta utata kati ya mkali wa Nipakate, Otile Brown na aliyekuwa maneja wake Dokta Eddie, Otile Brown ameamua kosonga mbele kinamna yake.

Tayari ameingia studioni na kutengeneza kitu na producer Haji huku nyimbo hiyo itakapodondoka itadondoka pamoja na video yake kwa mpigo. Juzi alisema kuwa yeye hana haja ya kusumbuana na Dr. Eddie maana tayari ameshaachia wakili wake kesi ya kuhusu kutozitumia ngoma zake za awali mpaka atakapolipa deni la mamilioni ya pesa taslimu zenye thamani ya Kenya ambazo Eddie hajaweka wazi ni ngapi.

Otile hata hivyo, Jumatano hii amewatoa wasiwasi mashabiki wake na wadau wa muziki kwa kuikonyeza post za matumaini mapya kwenye mtandao wa Facebook kuandika, “#YuleMbaya Tarehe 21 Juma nne hii ijayo .. hakikisha ume subscribe kwenye YouTube channel yangu upate kua kati ya wale wa kwanza kujua pindi inapo dondoka.Hebu pata ku subscribe kwenye channel yangu ya Youteube .. #YuleMbaya Eneza Ujumbe share . share .share”

Makala ya: changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents