Michezo

Ozil: Mashabiki wanataka nibaki na sasa ni uamuzi wa klabu

Mchezaji wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil amesema kuwa yuko tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo lakini anataka kujua kama kocha wa timu hiyo Arsene Wenger atabaki kwenye klabu hiyo baada ya mwisho wa msimu huu.

Wenger ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni wa msimu huu wakati mikataba ya Ozil na Sanchez inamalizika baada ya miezi 18.

Ozil amefungka kuwa anafurahi sana kubaki kwenye klabu ya Arsenal na amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa angependa kuongeza muda wa mkataba wake.

“Nina furaha sana ndani ya Arsenal na nimeiacha klabu itambue hilo kwamba nipo tayari kusaini mkataba mpya.”Alisema Ozil wakati akiongea na waandishi wa habari za michezo za Ujerumani.

“Mashabiki wanataka nibaki na sasa ni uamuzi wa klabu.

“Wanajua kwamba nipo hapa kwa sababu ya Arsene Wenger. Yeye ndiye aliyenileta na yeye ndiye anayeamini nilichonacho. Klabu pia inajua kwamba nataka kuwa muwazi na kile meneja anataka kufanya.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents