Burudani

P Funk ashangazwa na Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa, ‘Hivyo tunacheza taarab’

Producer mkongwe Bongo, P Funk Majani amefunguka kuhusu kuwepo kwa beef miongoni mwa ma-producer wapya wa sasa.

P Funk ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wao kama ma-producer wanaheshimiana na suala la malumbano mara nyingi ni kwa wasanii na si kwao kwani kwa upande wa production wapo wachache.

“Labda hao wadogo ambao juzi kati nimeona wanalumbana, sijui S2kizzy, T Touch na Luffa, sijui wanasema muziki wa T Touch wa kizamani, hitu kama hivyo tunacheza taarab sasa,” amesema.

“Kwa sababu kinachoonekana ni kazi, kama muziki umekubali basi ni mzuri uwe wa kizamani au wa kisasa,” amesisitiza.

Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa ni ma-producer ambao kwa sasa kila mmoja anafanya vizuri hapa Bongo, wote kwa sasa ngoma walizofanya vinafanya vizuri katika radio station mbali mbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents