Habari

P-Funk: Mangwea alijiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya kupunguza mawazo

Producer P-Funk Majani amefunguka na kusema kuwa marehemu Albert Mangwea alijiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya ili kupunguza mawazo. Majani amesema kwa muda mrefu alikuwa akijaribu kumweka chini Mangwea kumuonya kuhusu matumizi ya madawa hayo lakini alikana kuyatumia.

IMG_1375

Ameongeza kuwa anajilaumu kwakuwa alishindwa kufanikiwa kumuondoa rapper huyo kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

“I knew already from 2006 kulikuwa na watu wanaongeaga kwamba anatumiaga madawa ila kila nikimkadamiza nimweke kwenye kiti nimwambia Ngwair you are using ‘ohh P don’t bring that shit you are accusing me and I always said ‘Ngwair come on’, amesema Majani kwenye video aliyorekodiwa na mtandao wa GongaMX.

“Kumbe miaka yote hiyo maskini alikuwa anatumia. Na I look in myself and I ask myself what is the reason for him to do this it was because psychologically he was unstable. Mangwea ni mtu ambaye amefanya vitendo vikubwa hapa nchini lakini ile faida na support a ukweli hajaipata,” aliongeza.

“Ukiangalia wasanii wengine wa Bongo Records akina Juma Nature, Profesa Jay they got more leverage but Mangwea was a very big artist, he made one of the best ever albums in Tanzania till to date. I think that’s what drove him slowly in depression and people don’t use drugs unless they are depressed. Kwasababu mimi situation kama hiyo ilishawahi kunifikia.”

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents